Kilimanjaro Yataja Majina ya Wafanyabiashara wa Dawa za Kulevya

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akizungumza juu ya msako mkali ulioanza wa kuwakamata wafanyabiashara wa dawa za kulevya katika mkoa wa Kilimanjaro.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad Mutafungwa akitaja majina ya watu wanadaiwa kujihusisha na usafirishaji, uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akinyunyiza marashi juu ya Mirungi iliyofungwa katika vipande vya magazeti ikiwa ni mbinu mpya inayotumiwa na wasafirishaji wa bidhaa hizo.
Baadhi  ya watuhumiwa wa dawa za kulevya waliokamatwa katika msako uliofanyika kwa muda wa siku nne.
Sehemu ya Misokoto ya Bhangi iliyokamatwa wakati wa opereshni hiyo .
Na Dixon Busagaga
 
JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limetaja majina ya watu 47 wanaotuhumiwa kuhusika
katika  kusafirisha, kuuza na kutumia dawa za kulevya huku likifanikiwa kukamata misokoto 269 na miche 13 ya Bhangi, pamoja na kilogramu 32.9 za mirungi pia ikikamatwa.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao pamoja na dawa hizo za kulevya kunatokana na msako mkali uliofanywa na kikosi maalumu cha jeshi hilo kwa muda wa siku nne katika maeneo
mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro.
Akitangaza majina hayo ofisini kwake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna
Mwanadamizi Msaidizi wa Polisi,Wibroad Mutafungwa alisema watuhumiwa hao tayari
wamekamatwa na wako katika hatua mbalimbali za kiupelelezi na taratibu zikikamilika watafikishwa mahakamani.
Miongoni mwa watuhumiwa 47 wamo watoto wawili  waumri wa miaka 17 ambao ni Wilfred
Mnubi mkazi wa Bomang’ombe wilaya ya Hai na Ruben Bakari mkazi wa Njoro katika
manispaa ya Moshi.
Kati ya watuhumiwa hao wanawake ni 15 na wanaume ni 32 akiwemo mzee mwenye umri wa
miaka 60, Christina Ferdinand.
“Vita hii tumeianza tangu mwaka juzi, tunajua vita hii ni kubwa bahati nzuri ni kwamba
njia wanazotumia wafanyabiashara wa dawa za kulevya husani mirungi na bhangi, tayari jeshi la polisi limezibaini, maeneo ambayo dawa za kulevya zimekithiri Jeshi la polisi limekwisha baini, operesheni hii ambayo tumeianza ni endelevu na tutaendelea kuwakamata watu hawa kwa kutumia mbinu zote tulizonazo.” alisema Mutafungwa
Waliotajwa na kushikiliwa na jeshi la Polisi ni pamoja na:
(1)
Juma
Kabwele(25).
(2)
Mohaed
Kabwele (29) .
(3)
Shabani
Mponda(39).
(4)
Khadija
Mushiri(27).
(5)
Veronika
Chuwa (39).
(6)
Mwanahamis
Hussein.
(7)
Yusuph
Issa(42).
(8)
Salim
Massawe(48).
(9)
 Hadija Mohamed(50).
(10)
Shenein
Abilah(41).
(11)
Husna
Mgonja(24).
(12)
Najima
Desouza (46) .
(13)
Ruben
Bakari (17) .
(14)
Paul
Kisoka (26).
(15)
Raphael
Mbuya (40).
(16)
Wilfred
Mnubi(17).
(17)
Athuman
Swaehe (35).
(18)
Joseph
Hamis(20).
(19)
Zuber
Temu(27).
(20)
Robert
Kitika (18) .
(21)
Mohamed
Juma (25).
(22)
 Ahmad Shaban (57).
(23)
Donas
Masashua(22).
(24)
Japhet
Tungai (46).
(25)
Asima
Mndeme (24).
(26)
Muutaz
Zalia ,
(27)
Noah
Singano (29).
(28)
Ramadhan
Masale (40) .
(29)      Kirambati
Swai(45).
(30)      Said
Mrii.
(31)      Erick
Henry (20).
(32)      Seif
Ally(20).
(33)      Ramadhan Hassan (36).
(34)      Victor
John(22).
(35)      Upendo Endkia (42).
(36)      Asia
Ally(39).
(37)      Catherine
Linusi (36) .
(38)      Mariam
Hemed (44) .
(39)      Mwajuma
Msuya (48).
(40)      Juma
Yusuph (22) .
(41)      Hussein
Anyokisye (17).
(42)      Musa
Msangi (30).
(43)      Ramadhani
Hassan (36).
(44)
Wilfred
Munubi(17)
(45)       Ruben Bakar.(17)
(46)       Christina
Ferdinand.(60)
(47)       Samweli
Kingai(42).
Mwisho