Wizara ya Fedha Yatekeleza Agizo la Magufuli, Yamlipa Mkandarasi Terminal 3

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akizungumza na Wanahabari..

 

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akizungumza na Wanahabari kuhusu Wizara yake ilivyotekeleza Agizo la Rais Dkt. John Magufu kuhusu kumlipa Mkandarasi anayejenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3).

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Doto James, Wizara ya Fedha na Mipango imemlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3) Kampuni ya BAM International kiasi cha Euro Milioni 9.5 sawa na zaidi ya Tsh. Bilioni 22 za Kitanzania mara baada ya kuhakiki madai hayo.

Katika Hatua nyingine Wizara ya Fedha inaandaa Malipo ya awali (Advance Payment) kiasi cha Tsh. Bilioni 300 kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Kutumia Umeme na Mafuta (Standard Gauge) katika awamu ya kwanza itakayoanzia kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro katika awamu yake ya kwanza ya Ujenzi huo. Picha na Mpiga picha Wetu