Na Emanuel Madafa, Mbeya
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametoa siku 14 kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuhakikisha inawaondoa watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi za misitu pamoja na hifadhi ya misitu ya Mlima Mbeya.
Aidha amesema agizo hilo pia liendane na suala la kudhibiti shughuli zote za kibinadamu kando kando ya mita 60 kwa kufuata sheria ya mita 60. Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa agizo hilo katika kilele cha upandaji miti kimkoa katika eneo la chanzo cha maji cha mto Hanzya kata ya Itagano jijini Mbeya.
Amesema lazima agizo hilo litekelezwe mapema sanjali na kufanya tathimini ya hali yauhalibifu wa mazingira katika maeneo yote.
“Nikazi bure kuendelea kupanda miti wakati ile iliyopandwa mwaka uliopitwa imehalibiwa kwa kukosa matunzo au kuhalibiwa kwa shughuli za kibinadamu,“Alisema Makala.
Aidha Makalla ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupanda miti ya vivuli na matunda kwenye maeneo yao hususani katika maeneo ya vyanzo vya maji kwani ni muhimu kwa maisha ya kila siku.
“Serikali imeweka lengo la kupanda miti isiyopungua milioni 1 kwa mwaka katika kila halmashauri mkoani humo ambapo mwezi juni mwaka huu kufanyika tathimini ya pamoja kuona zoezi hilo lilipo fikiwa,“Alisema
Naye Afisa Misitu Mkoa wa Mbeya Ndugu Joseph Butuyuyu mpango wa kuhifadhi safu ya Mlima Mbeya umeanza kwa mafanikio makubwa hasa kutokana kuungwa mkono na waziri mwenye dhamana ya Mazingira Ndugu January Makamba mara baada ya kutembelea safu ya Mlima huo.
Wananchi wa kijiji cha Hanzya kata ya Itagano wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla katika kilele cha Upandaji Miti Kimkoa katika SAFU ya Mlima Mbeya January 31 ,2017 |
Mkutano ukiendelea……… |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipanda mti katika kilele cha Upandaji kimkoa katika chanzo cha Maji Hanzya Kata ya Itagano. |