Soko la Big Brother Manzese Dar lavunjwa

Kwa waliowahi kufika Dar es Salaam wanaweza kuwa wanalifahamu soko maarufu la mitumba linaloitwa kwa jina maarufu la Big Brother limevunjwa na sasa wafanyabiashara takribani elfu tatu waliokuwa wakiendesha biashara eneo hilo wanahaha kutafuta eneo lingine. Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia, FFU walilazimika kuwatawanya wafanyabiashara hao kwa mabomu na risasi hewani walipotaka kufunga barabara siku moja baada ya maeneo yao kuvunjwa siku.