Vijana hao waliofanikiwa kuchaguliwa kuwa mabalozi wa “CHAMPION FOR CHANGE” ni Agnes Mgongo, Doris Mollel, Hassani Tozir, Catherine Ruge pamoja na Sadick Lungendo.
Mabalozi hawa watashirikiana na serikali kwa kwa hamasa na mafunzo mbalimbali ili kuwainua na kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi.
Hivyo basi wadau wote kwenye njanja tofauti tofauti wanaombwa kuwaunga mkono mabalozi hawa kwa kushiriki kwenye midahalo au mahojiano kwa kupitia kwenye mtandao mkubwa kijamii ulioanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) unaoitwa “JOIN THE MOVEMENT” kwa kufuatisha kiunganishi (link) hapa chini kujisajili na kuanzisha mijadala yako.
https://www.empowerwomen.org/en/join-the-movement