Zanzibar Wajitokeza Kutembelea Banda la NIDA Viwanja vya Maisara

Wananchi wakijisajili kwenye kitabu cha wageni walipofika kutembelea banda la Maonesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) viwanja vya Maisara Zanzibar.

Wananchi wakijisajili kwenye kitabu cha wageni walipofika kutembelea banda la Maonesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) viwanja vya Maisara Zanzibar.

. Shau Mwalim Haji akimsajili mwananchi aliejitokeza katika maonyesho ya Biashara ya Maisara.

. Shau Mwalim Haji akimsajili mwananchi aliejitokeza katika maonyesho ya Biashara ya Maisara.

Wafanyakazi wa NIDA wakiwa katika picha ya pamoja, wakijipanga katika Banda la maonyesho hapo katika viwanja vya maonyesho vya Biashara vya Maisara Zanzibar ili kuhudumia wananchi watakaohudhuria.

Wafanyakazi wa NIDA wakiwa katika picha ya pamoja, wakijipanga katika Banda la maonyesho hapo katika viwanja vya maonyesho vya Biashara vya Maisara Zanzibar ili kuhudumia wananchi watakaohudhuria.

WANANCHI wa Zanzibar wamejitokeza kwa wingi kwenye sherehe za uzinduzi wa maonesho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yanayoendelea kwenye viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.

Maonesho hayo yamezinduliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, ambaye pamoja na mambo mengine amesisitiza Taasisi za Serikali na binafsi kutumia vema fursa ya maonesho kujitangaza na kuonyesha shughuli wanazofanya kwa wananchi.

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ni miongoni mwa Taasisi zinazoshiriki maonesho hayo ambapo pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa Vitambulisho, inaendesha zoezi la kusajili wananchi ambao bado hawajasajiliwa, kugawa vitambulisho vya Taifa kwa wananchi waliokamilisha taratibu za usajili, pamoja na kuonesha mfumo salama (tovuti) inayotumika kusoma taarifa za mtu zilizoko kwenye mfumo kwa njia ya mtandao. Njia hiyo itawezesha wadau mbalimbali kutumia mfumo huo kuhakiki taarifa za mwananchi mwenye kitambulisho kabla ya kumpatia huduma.

Kaimu Meneja wa kitengo cha Operesheni Zanzibar Ndg. Abdala O. Mmanga akitoa elimu juu ya matumizi ya Vitambulisho Vya Taifa kwa wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Maonyesho vya Maisara ZanzibarKaimu Meneja wa kitengo cha Operesheni Zanzibar Ndg. Abdala O. Mmanga akitoa elimu juu ya matumizi ya Vitambulisho Vya Taifa kwa wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Maonyesho vya Maisara Zanzibar.

Banda la NIDA limekuwa moja ya mabanda ya kuvutia, ambapo wananchi wengi wamekuwa wakitembelea shughuli mbalimbali zinazoendelea kwenye viwanja hivyo na kuonekana kuridhishwa na huduma zinazotolewa na NIDA.
Maonesho ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yameanza tangu Jumamosi tarehe 07 Januari 2017 yakihusisha Taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Taasisi za Muungano, mashirika na Taasisi binafsi na yanatarajiwa kumaliza Jumamosi tarehe 14/01/2017.