Dk. Bilal azungumza na Waziri wa Maendeleo Sweden

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sweden, Gunilla Carlsson, wakati alipofika ofisini kwake kwa mazungumzo jijini Stockholm Sweden juzi.

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akichangia katika kongamano la lililoandaliwa na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sweden, Gunilla Carlsson, kuhusu nafasi ya uhusiano wa Tanzania na Sweden, lililofanyika jijini Stockholm Sweden juzi.

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya picha yenye Taswara ya mjini wa Zanzibar, Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sweden, Gunilla Carlsson, wakati Makamu alipofika Ofisini kwa waziri huyo jijini Stockholm Sweden kwa mazungumzo juzi. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR