Baadhi ya wanakijiji wa same wakipata huduma ya maji safi na salama kwa mara ya kwanza.
|
Baadhi ya wanakijiji wa same wakipata huduma ya maji safi na salama kwa mara ya kwanza |
KAMPUNI ya Bia Serengeti leo imezindua mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 83 katika eneo la Makanya wilayani Same ikiwa ni jitihada za kuwaletea maji safi na salama wakazi wa eneo hilo. Ukiwa na uwezo kwa kuhudumia watu 10,629, mradi huo unajumuisha kisima pamoja na mifumo yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la maji ambapo zinazalishwa lita 20,000 za maji kwa kila saa moja.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha alisema kuwa mradi huo ambao unajulikana, “Maji kwa Uhai” ni mionmgoni mwa mikakati kama hiyo ambayo kampuni hiyo ya bia imeiendesha katika mikoa ya Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwa inawanufaisha zaidi ya watu milioni moja kwa maji safi na salama.
Wanyancha alisema kwamba mradi wa Makanya sio tu kwamba utaboresha afya za wakazi wa eneo hilo bali pia utaongeza tija katika kiuchumi, “hususani kwa watoto wa kike na wanawake ambao hawatahitaji kutumia saa nyingi kutafuta maji safi sehemu nyingine. Hii inawapa fursa ya kuhudhuria shule wakiwa huru.”
“SBL ina sera iliyojikita katika ustawi wa jamii yetu na Maji kwa Uhai ikiwa ni mojawapo ya maeneo manne ya kipaumbele ambayo kampuni yetu imeyabainisha katika lengo lake kuipatia jamii msaada katika jumuia inamohudumia”, alisema Wanyancha akielezea vipaumbele vingine hivyo kama: Kutoa Stadi za Maisha, Undelevu wa mazingira na Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.
Mkurugenzi huyo wa mahusian0 aliendelea kusema SBL ina programu ya kilimo ambayo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imewasaidia wakulima zaidi ya 100 nchini kwa kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha iliyowasaaidia kuboresha maisha yao na maisha ya jumuia zao.
Wanyancha alisema kutokana na juhuzi hizo, “SBL imeweza kuibua tani za malighafi inazotumia kutoka wa wakulima wa hapa nchini kutoka 0 hadi tani 1000 na hili limechangia katika kukua kwa kampuni na kukuza kipato cha wakulima.”
Aliendelea kubainisha: “Licha ya kuchangia katika kukua kwa uchumi wa taifa kupitia malipo ya kodi ya mara kwa mara, SBL imetoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa hususani katika kutoa huduma ya maji safi na salama ndani ya nchi.”
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule aliipongeza SBL kwa kutoa msaada uliokuwa unahitajika mno, akisema kwamba kampuni hiyo ya bia imekuwa mstari wa mbele katika kukuza miradi ya maendeleo nchini ambayo inawezesha kuwepo kwa jamii inayozalisha na iliyo na afya.