Waziri Mkuu Majaliwa Azindua Mradi wa Umwagilia

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua mradi wa maji uliofadhiliwa na shirika la World Vision wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa miradi wa shirika hilo Devocatus Kamara ,mradi huo uko katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karatu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua mradi wa maji uliofadhiliwa na shirika la World Vision wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa miradi wa shirika hilo Devocatus Kamara ,mradi huo uko katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karatu

Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amezindua mradi wa Umwagiliaji katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karatu uliofadhiliwa na Shirika la Word vision ambao unahudumia ekari 1200 na kuwafikia wakulima 4000.

Akizungumza katika uzinduzi wa Mradi huo ,Majaliwa amesema kuwa mradi huo utasaida kuchochea kilimo cha umwagiliaji hasa katika kipindi hiki ambacho kuna mabadiliko ya tabia ya nchio na uhaba wa mvua.

Majaliwa amesema kuwa Asilimia 80% ya Watanzania wamejiajiri katika sekta ya kilimo idadi ambayo ni kubwa hivyo kilimo cha umwagiliaji kikihamasishwa ipasavyo wakulima watapata tija kubwa na kuinua pato la taifa.

Aidha amelishukuru shirika la Word vision kwa kujitoa kusaidia jamii katika eneo hilo muhimu la kilimo ambalo ni tegemeo kwa wakulima wengi.

Waziri Mkuu ameonya tabia ya baadhi ya watu wanaohujumu vyanzo vya maji kwa kuunganisha mashine katika vyanzo na kufanya uharibifu hivyo amewataka kuondoka mara moja katika chanzo hicho na iwapo watakaidi serikali itawachukulia hatua kali.

Mkurugenzi wa Miradi katika shirika la World Vision Revocatus Kamara amesema kuwa mradi huo utawanufaisha wakulima wengi na kupelekea upatikanaji wa chakula pamoja na kukuza kipato cha wakulima.

Kamara amesema kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana vyema na serikali ili kufanya miradi itakayosaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii.