Taasisi ya ANSAF Yawanoa Wadau wa Kilimo Kanda ya Ziwa

Jimmy Luhende ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini, akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa Kilimo Kanda ya Ziwa.

Jimmy Luhende ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini, akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa Kilimo Kanda ya Ziwa.

Katibu Tawala Msaidizi idara ya Uchumi na Uzalishaji mkoani Mwanza, Joanen Kukwami akifungua mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, 
Mkutano huo uliandaliwa na Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuhakikisha kunakuwa na kilimo chenye tija katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili familia ziweze kujikimu kiuchumi na kichakula.
Meneja Mradi wa Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, Diana Lugano, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, jana Novemba 03 na leo Novemba 04, 2016.
Mratibu na Mchambuzi wa Sera na Bajeti kutoka Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, Joseph Nyamboha, akiwasilisha mada kwenye mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza, akijitambulisha.
Washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza akichangia mada.
Mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza akichangia mada.
Picha ya pamoja
************************************************
Upungufu wa maafisa kilimo pamoja na uuzaji wa mbegu zisizo na ubora katika mikoa ya kanda
ya ziwa umeelezwa kusababishwa sekta ya kilimo katika mikoa hiyo kuzorota.
Hayo yalibainishwa jana Jijini Mwanza kwenye mkutano wa wadau wa kilimo uliolenga kujadili
namna bora ya kuboresha sekta hiyo.
Walisema baadhi ya maafisa kilimo waliopo katika mikoa ya kanda ya ziwa kushindwa
kuwafikia wakulima na kuwapatia elimu ya kilimo husababisha kilimo kisicho na
tisha huku uuzaji wa mbegu za kilimo zisizoota ukikwamisha kabisa juhudi za
wakulima kulima zao hilo.
Mkutano huo uliandaliwa na Jukwaa la wadau wa kilimo nchini ANSAF na kuwakutanisha wadau
mbalimbali wa kilimo wakiwemo wakulima, viongozi wa serikali pamoja na taasisi
binafsi ambapo pamoja na mambo mengine umeadhimia kufikisha elimu kwa wakulima
ili kulima kilimo chenye tija.