Mourinho, Moyes Wapigwa Rungu na FA

david-moyes

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameshtakiwa na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kudai kwamba itakuwa vigumu kwa refa Anthony Taylor kusimamia mechi yao dhidi ya Liverpool.

Mourinho aliongezeawamba kumteua Taylor kusimamia mechi hiyo ya tarehe 16 Oktoba ilimpatia shinikizo refa huyo mwenye makao yake Manchester. Mameneja hawaruhusiwa kuzungumzia kuhusu marefa kabla ya mechi.

Mourinho ana hadi Oktoba 31 kujibu shtaka la ukosefu wa nidhamu na kusababisha mechi hiyo kuwa na jina baya. Taylor alito kadi 4 za njano zote kwa timu ya Manchester United katika sare hiyo ya 0-0
Naye Meneja wa klabu ya Sunderland ya Uingereza David Moyes ameshtakiwa na chama cha soka cha Uingereza kwa utovu wa nidhamu wakati wa mechi dhidi ya Southampton Jumatano.

Southampton walishinda mechi hiyo ya Kombe EFL Cup uwanjani St Mary’s kupitia bao la Sofiane Boufal

Chama cha Soka cha Uingereza (FA) kimesema inadaiwa “Moyes alitumia lugha ya kutusi au maneno ya kuudhi akiyaelekeza kwa mwamuzi wa mechi.”
Kisa hicho kilitokea dakika ya 90 refa Chris Kavanagh alipokataa kuwapa Sunderland penalti baada ya mshambuliaji wa Sunderland Victor Anichebe kuonekana kuchezewa visivyo eneo la hatari, Sunderland walilazwa 1-0.