OKTOBA 29, 2016, wakazi wa Mwanza kwa mara ya kwanza watapata fursa ya kushuhudia msisimko wa mashindano ya ulimbwende ya Miss Tanzania ambapo washiriki 30 watapanda jukwaani kushindania nafasi ya kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano hayo ya dunia yatakayofanyika Disemba 18, 2016 jijini Washington DC, Marekani.
Tukio hili litakalofanyika kwa mara ya kwanza mkoani humo litakuwa ni lenye msisimko mkubwa ambapo fursa nyingine pia za mkoa huo zinaweza kutangazwa mbali na kuwa kitovu cha shughuli za biashara na burudani ukiachana na mkoa wa Dar es Salaam. Meneja Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania Bi. Fatema Dharsee, kampuni inayojihusisha na huduma za hoteli kwa njia ya mtandao amesema kuwa wao wameliona tukio hilo kama sehemu ya kupaza sauti kwa wageni watakaokwenda Mwanza kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii ambavyo wengi wao hawavijui.
“Oktoba 29 ya Jumamosi hii litafanyika shindano la Miss Tanzania ambalo huwa linavutia wadau wengi katika sekta ya burudani na utalii kwa ujumla. Sisi kama Jumia Travel Tanzania tumeona kuwa kuna mambo mengi ya kufanya na kufurahia mbali na kushuhudia tukio hilo. Jiji la Mwanza au ‘Rocky City’ kama linavyojulikana na watanzania wengine hasa kutokana na asili ya ardhi ya mkoa huo kuwa na mawe makubwa ambayo ni kivutio kikubwa cha kwanza kwa yeyote atayetembelea kwa mara ya kwanza.” Alisema Bi. Dharsee
“Mbali na mawe hayo yaliyotapakaa karibuni jiji zima hususani yale maarufu yanayojulikana kwa jina la ‘Mawe ya Bismarck’ ambayo umaarufu wake na kutumika kama nembo ya utambulisho ya mkoa huo ni namna yalivyobebana. Mwanza inavyo vivution vingi vya watalii kama vile makumbusho ya Kageye, ambayo ni mojawapo ya makumbusho kongwe kabisa nchini Tanzania. Ukitembelea Kageye utajionea masanamu ya waafirka ambao walichukuliwa utumwani enzi za biashara hiyo ambapo mwaka 1994 UNESCO ilitangaza kama mojawapo ya tukio kubwa la kutekezwa kwa Waafrika. Pia katika makumbusho haya utaweza kujua kazi mbalimbali zilizofanywa na wapelelezi waliotumwa na wakoloni kupeleleza bara la Afrika kama vile Henry Morton Stanley, Dr. Fisher, Dr. Junker, Sir Richard Frencis Burton na John Speke.” Aliongezea zaidi Bi. Dharsee
Mbali na makumbusho hayo pia ukifika Mwanza unaweza kufurahia safari ya kwenda kutembelea kisiwa kikubwa cha Ukerewe. Kisiwa hiki kinaweza kufikika kiurahisi kupitia makao yake makuu ya ofisi zilizopo mji wa Nansio. Pia jambo lingine ambalo watu hawalifahamu ni kwamba ukiwa Mwanza unaweza kwa urahisi kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ipo umbali wa takribani masaa mawili tu. Mbali na Serengeti, jiji hilo pia lipo karibu na Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ambapo kuna aina ya kipekee ya sokwe wanaopatikana.
“Jiji la Mwanza pia kama mikoa mingine lina tamaduni zake kama vile ngoma za asili, lugha, shughuli na vyakula vyao. Wageni watakaotembelea mkoa huo nawasihi wafanye jitihada za kutembelea ‘Kambi ya Utamaduni’ ambayo inapatikana kilometa 12 kutokea lango la kuingilia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Hapa unaweza kufurahia uvuvi, na safari za kwenye mtumbwi zinazoongozwa na wenyeji wa pale kwa kutumia majahazi na mashua. Pia utafurahia ngoma maarufu ya asili ya Wasukuma inayojulikana kama ‘Igobogobo’, ngoma za kucheza na moto au nyoka na vilevile nyimbo za asili. Mwisho kabisa utakuwa hujalifaidi jiji la Mwanza kama hautopata fursa ya kula samaki watamu aina ya Sato na Sangara ambao wanapatikana Ziwa Victoria pekee la mkoani hapo.” Alihitimisha Meneja huyo Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania.
Kuhusu Jumia Travel
Jumia Travel (travel.jumia.com) ni mtandao nambari moja unaongoza wa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao wenye orodha ya hoteli zaidi ya 25,000 kwa nchi za Afrika na zaidi ya hoteli 200,000 duniani kote. Dhumuni letu ni kuleta kila aina ya huduma za malazi kwenye mfumo wa mtandao na kutengeneza njia rahisi na nafuu zaidi kwa wateja kuzilipia.
Hapa Jumia Travel, tunao mamia ya wataalamu katika masuala ya utalii ambao huwasiliana na wateja wetu. Ofisi zetu zinapatikana katika miji na nchi zifuatazo Lagos (Naijeria), Accra (Ghana), Dakar (Senegali), Abidjan (Ivory Coast), Algiers (Algeria), Douala (Cameroon), Kampala (Uganda), Dar Es Salaam (Tanzania), Nairobi (Kenya), Addis Ababa (Ethiopia), Porto (Ureno) na Paris (Ufaransa). Kabla ya mwezi Juni mwaka 2016, Jumia Travel ilikuwa ikijulikana kama Jovago. Ilianzishwa mwaka 2013 na Jumia ambayo inaendeshwa kwa kushirikiana na MTN, Rocket Internet, Millicom, Orange na Axas kama washirika wao katika masuala ya kifedha.