Na Woinde Shizza, Arusha
MWANDAAJI wa Tamasha la Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Mwandago Entertainment Ltd,Faustine Mwandago ametangaza kujiondoa rasmi kuandaa tamasha hilo huku akitaja sababu iliyompelekea ni pamoja na ubabaishaji uliojaa ndani ya mashindano hayo.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani hapa Mwandago alisema kwamba ameamua kuchana na kuandaa tamasha hilo kutokana na hali ya ubabaishaji iliyokithiri ndani ya mashindano hayo.
“Nimeamua kuachana na kuandaa tamasha hili kwa kuwa kuna mambo ya ubabaishaji mwingi ndani yake kadri ya siku zinavyokwenda
mambo yamekuwa na ubabaishaji sana umesikia hata Mwanza yaliyotokea yanakatisha tamaa,” alisema Mwandago
Alisema kwamba mbali na sababu hiyo jambo jingine lililompelekea kuachana na uandaaji wa tamasha hilo ni pamoja na uhaba wa
wadhamini ambao umeshuka kwa kikubwa na kupelekea kudhohofisha mashindan0 hayo. Mwandago,alisema kwamba lakini pamoja na kuachana na kuandaa tamasha hilo atakuwa bega kwa began a mshiriki wa taji hilo kanda yaKaskazini katika safari yake na kumtaka mlimbwende huyo kutokuwa na wasiwasi.
“Pamoja na kwamba nimeamua kuachana na kuandaa tamasha hili lakini mrembo anayewakilisha kanda ya kazkazini ambaye nilisimamia
uteuzi wake nitaendelea kumpa sapoti katika safari yake bila wasiwasi,” alisema Mwandago.