Kila Mtu Ana Deni la Kulipa Hata Kama Hujakopa

hela

Na; Ferdinand Shayo

Kila mtu duniani ana deni la kulipa hata kama hudaiwi na benki,vikoba ama mtu binafsi bado duniani inakudai .Inakudai kwasababu umekuja duniani na kitu maalumu ambacho unapaswa kukitoa duniani ili kilete manufaa fulani.

Tumezaliwa tuko duniani kuijaza dunia na kuipa dunia vitu ambavyo dunia haina ,vitu vipya na vya kitofauti na vya kiubunifu.Fikiri Hapo zamani dunia ilikua haina vitu vingi kulikua na ardhi,mimea ,miti na wanyama binadamu alitumia malighafi hizo kutengeneza dunia kuwa sehemu bora ya kuishi kuliko alivyoikuta.

Juhudi hizo ndizo zilizofanya dunia kuwa bora na kuboresheka siku baada ya siku ,wagunduzi na wakandarasi wakajengo makubwa yaliyovunja rekodi duniani ,wakaijaza dunia majengo makubwa,wagunduzi wa simu wakaijaza dunia simu ,kompyuta na bidhaa mbali mbali za kielektroniki ambazo mwanzo hazikuwepo.

Waimbaji,Wanamuziki na Waigizaji wakiajaza dunia nyimbo nzuri,filamu ,Waandishi wa vitabu nao wakijaza dunia vitabu na maarifa mbalimbali yaliyotoka katika mioyo yao na vichwa vyao.

Fikiri umekuja kuijaza nini dunia? ,umekuja kuilisha nini dunia? maana dunia ina njaa inahitaji sana kitu ulichonacho jitaidi ukitoe dunia itashiba na itakua sehemu bora za kuishi kuliko ulivyoikuta.

Dunia inakutegemea wewe kuliko wewe unavyoitegemea ndio maana mtu akifa hajatuimiza kusulida ya yeye kuwepo duniani anaiacha dunia katika hali ya ukiwa.

Usipotimiza kusudi la wewe kuwepo duniani mara nyingi ndani ya nafsi yako na moyo wako utahisi una deni kuna kitu ulipaswa kukifanya duniani lakini hujakifanya.

Unapohisi madeni ndani yako huwezi kupata amani ya moyo mara nyingi utapata msongo wa mawazo ama stress mpaka ulipe deni kwa kufanya kitu ambacho unatakiwa ukifanye duniani.

Mimi sijui wewe umekuja duniani kufanya nini lakini kila mtu aliyoko duniani ana kusudi maalumu hakuna mtu aliyekuja duniani kwa bahati mbaya au kama kasha tupu lisilo na kitu.

Dunia inahitaji sana kitu ulichonacho ,dunia ina njaa ,dunia inateseka kwa sababu wewe hufanyi kitu ambacho ulipaswa kufanywa ,na kuna watu wanapata shida kwasababu yako inawezekana maisha yako yamekusudiwa kugusa maisha ya watu wengi ukiwa mbinafsi watu wengi watateseka kwa ajili yako.

Dunia ina nafasi ya kila mtu kufanya kitu alichokusudiwa kufanya kufanya duniani .Usipofanya hicho kitu mpaka unaingia kaburini utaacha nafasi iliyo wazi duniani.

Linapokuja suala la kutimiza kusudi la maisha yako dunia inakutazama wewe na si mtu mwingine,haiangalii makundi makundi ni suala la mtu binafsi na muito wake unamuita kufanya jambo ambalo linayapa maisha yake maana na thamani.

Ukweli ni kwamba uko duniani peke yako ,pale unapokua na watu ndio unakua nao lakini uko duniani peke yako Hupaswi kuishi maisha kwa kufuata mkumbo ,kusudi la maisha yako ni la kipekee sana halifanani na la mwingine hata ratiba zako lazima ziwe za tofauti zinaweza zisifanane na za mwingine hilo lisikutishe wala lisikuogopeshe.

Jua kwamba Wewe ni mtu wa tofauti na wa kipekee uko duniani ili ufanye vitu vya tofauti usipende kufanya vitu vya kawaida kawaida utaishia kuwa mtu wa kawaida ,familia ya kawaida,uchumi wa kawaida ,maisha ya kawaida.
Kataa kuwa mtu wa kawaida ni haki yako kuwa mtu wa tofauti kwa sababu hakuna mtu kama wewe duniani wewe ni wakipekee na kitofauti hata alama zako za vidole (finger print ) hazifanani na mtu yoyote duniani hata wataalamu na wanasayansi wamethibitisha.

Ishi maisha yako sasa timiza ndoto zako sasa acha kuishi maisha ya kuiga wengine wanafanya nini ,kuwa wewe kuna msemo wanasema “Kuwa Original” kuwa halisi usiwe feki.

Pata muda wa kukaa peke yako ,Kujitafakari wewe ni nani? Kwanini uko duniani? Umekuja kufanya nini? Itakusaidia kujitambua ,kutambua thamani yako na kitu ulichonacho.

Jitaidi sana usife na deni la kutimiza kusudi la maisha yako ,kutokutumia vipaji vyako,uwezo ulionao,maarifa uliyonayo kwasababu dunia inakudai.

Kama dunia inakudai ukifa na deni hutapumzika kwa amani kwasababu umeacha deni ,na mara nyingi watu wenye madeni hawana amani.

Kutimiza ndoto zako kutakupunguzia msongo wa mawazo kwasababu watu wengi wenye msongo wa mawazo ni wale ambao ndoto zao hazikutimia hazikuingia kwenye uhalisia.

Furaha,amani namafanikio yako kwenye kutimiza kusudi la maisha yako.

ferdinandshayo@gmail.com
0765938008
Maishayathamanitz.blogspot.com