Rais Magufuli Kununua Ndege Nyingine Mbili

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akipeana mkono na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamuhilo mara baada ya kuwekeana saini ya makabidhiano ya ndege mpya za abiria aina ya Bombadier- 8 Q400 zilizonunuliwa na Serikali kutoka nchini Canada, wakati wa hafla ya uzinduzi wa ndege hizo leo Jijini Dar es Salaam.

Na Sheila Simba, MAELEZO – Dar es Salaam

RAIS wa Tanzabia, Dk. John Magufuli amesema Serikali imejipanga kununua ndege mbili aina Jet zenye uwezo wa kubeba abiria 160 na 242 pamoja na kutenga Tsh. Bilioni 100 kwa ajili ya ukarabati viwanja vya ndege nchini.

Alisema hayo leo Jijini Dar Es Salaam wakati wa uzinduzi wa ndege mpya mbili za abria aina ya bombardier – 8 Q400 zilizonunuliwa na Serikali kutoka nchini Canada ,na kuongeza kuwa ndege hizo zitasaidia kuboresha sekta ya usafiri wa anga nchini.

“Ndege hizi ni nzuri sana, kwani ukitaka kujenga nchi yenye uchumi wa kisasa huwezi kujenga bila kuwa na ndege na ukitaka watalii lazima uwe na ndege” alisema Rais Magufuli. Alisema kuwa ndege hizo mbili zitakazonunuliwa na Serikali zitakuwa na uwezo wa kubeba kusaidia watalii kuja nchini moja kwa moja bila kutua nchi nyingine.

“Tunataka watalii wanaokuja nchini kuja moja kwa moja bila kushuka nchi nyingine ili kuongeza mapato yetu na kukuza utalii duniani na kuwa na ndege nyingi zaidi kama nchi nyingine,” alisema Rais Magufuli.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akiwekeana saini ya makabidhiano ya ndege mpya za abiria aina ya Bombadier- 8 Q400 baina yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamuhilo wakati wa hafla ya uzinduzi wa ndege hizo leo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ubora wa ndege za bombardier alisema kuwa ndege hizo zinaenda na mazingira ya hapa nchini na zina uwezo wa kutua katika viwanja vyenye lami na vile ambavyo havina lami na uendeshaji wake ni wa gharama nafuu.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema kuwa ndege za bombardier zinatumia mafuta kidogo ikiwemo gharama ya tsh Milioni 1 za mafuta kwa safari moja ikilinganisha na ndege nyingine zenye kutumia tsh. Milioni 28 kwa safari. Rais Magufuli aliitaka bodi ya shirika la ndege Tanzania (ATCL) kufanya kazi nzuri ya kusimamia ndege hizo na kutoa huduma nzuri na kuhakikisha wanapata faida ili serikali waweze kununua ndege nyingi zaidi.

Alisema kuwa bodi ya ATCL wana kazi kubwa ya kufanya kuboresha shirika hilo, kutokana na uzembe wa wafanyakazi wake kutokuwa makini na kuwataka kupanga vizuri safari za ngede hizo kwani zina uwezo wa kwenda mpaka nchi jirani.

“lazima mjue mnaingia kwenye ushindani na washindani wenu hawawezi kufurahia wapo hujuma ili shirika lisisonge mbele sasa fanyeni kazi,” alisema Magufuli.

Aidha amewaomba ATCL kutotumia mawakala katika kukatisha tiketi na kuzingatia muda wa safari ulipangwa na kutoa huduma nzuri kwa wateja wao ili kukuza utalii nchini na kuwaomba watanzania kuwa wazalendo kwa kutumia usafiri huo.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa alisema ndege hizo zilizozinduliwa zinauwezo wa kubeba abiria 76 na abiria 6 wakiwa ni wa daraja la biashara na 70 ni daraja la kawaida na ina uwezo wa kubeba mzigo wa tani moja.

Baadhi ya Malubani wa ndege mpya za Serikali aina ya Bombadier -8 Q400 zilizonunuliwa kutoka nchini Canada wakifualtilia kwa makini hotuba mbalimbali za Viongozi wa Serikali wakati wa hafla ya uzinduzi wa ndege hizo leo Jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa shirika la ATCL lina upungufu mkubwa wa watalaamu katika maeneo mbalimbali ikiwemo, marubani, wahandisi, wanasheria, maafisa biashara, wahasibu na menejimenti na hatua inayosabisha shirika hilo kushindwa kujiendesha vizuri.

Waziri Mbarawa alisema kuwa ATCL wamejipanga kutoa huduma za usafiri katika viwanja vya Dodoma, Dar Es Salaam Bukoba, Tabora, Zanzibar, Mbeya, Kilimanjaro, Mtwara, Mwanza Kigoma, Arusha na Comoro.