Wafanyabiashara Kariakoo Watoa Mil 60 kwa Waathirika Tetemeko Kagera

 Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mtaa Muhonda, Kariakoo, akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Philimon Chonde, fedha taslimi mchango kutoka kwa wafanyabiashara hao kwa ajili ya walioathirika  kwa tetemeko Kagera. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa JWK, Abdalah Mwinyi na Mweka Hazina wa jumuia hiyo, Silvanus Mande.

Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, akizungumza jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea michango ya fedha na vifaa kutoka kwa wanachama wa jumuia hiyo kwa ajili ya walioathirika kwa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.  Jumla walichanga fedha na vifaa vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 60.7.

Katibu wa JWK, Mtaa wa Raha Square, Frank Nduta akikabidhi vitenge na bidhaa nyingine kwa Mwenyekiti wa JWK, Philimon Chonde

Wafanyabiashara wa Mtaa wa Mchikichi Kariakoo, wakitoa msaada wa  misumari kwa ajili ya waathirika wa tetemeke, Kagera.

(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)