Celtic walipokezwa kichapo kibaya zaidi katika mashindano ya Ulaya Jumanne usiku baada ya kuchapwa mabao 7-0 na Barcelona uwanjani Camp Nou.
Mshambuliaji Lionel Messi, raia wa Argentina, alifunga ‘hat-trick’ yake ya sita katika mechi hiyo ya kundi C.Alianza kwa kufunga bao la mapema.
Mchezaji wa Celtic Moussa Dembele alishindwa kufunga penalti kabla ya Messi kufunga la pili. Kipindi cha pili, Neymar alifunga kupitia frikiki, Andres Iniesta akafunga la nne, Messi akaongeza la tano naye Suarez akakamilisha ushindi kwa mabao ya sita na saba.
Naye Alexis Sanchez aliwasaidia Arsenal kuondoka na alama moja mechi yao ya kwanza msimu huu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Paris St-Germain.
Edinson Cavani aliwaweka PSG mbele baada ya sekunde 42 pekee na alikuwa na nafasi ya kufunga mabao matatu kufikia muda wa mapumziko.