Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Saidiq akiwasili katika shule ya msingi Mandela iliyopo kata ya Bomabuzi wilaya ya Moshi kwa ajili ya kupokea msaada wa Madawati yaliyotolewa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Wanafunzi katika shule ya Msingi Mandela wakiimba nyimbo wakati wakipokea wageni waliofika katika tukio la kukabidhi madawati.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) Joyce Msiru akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq alipowasili katika shule ya msingi Mandela kwa ajili ya kukabidhiwa Madawati.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Saidiq akiwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba (kushoto) pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya (kulia) wakati wa makabidhiano ya Madawati kwa ajili ya shule ya msingi Mandela.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) ,Joyce Msiru akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi madawati kwa ajili ya shule ya msing Mandela.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiq (katikati) akiwa ameketi kwenye Dawati na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru pamoja na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mandela.