Klabu zilizovunja rekodi zao binafsi katika ununuzi
Manchester United: Paul Pogba (£89m) Bournemouth: Jordon Ibe (£15m)
Liverpool: Sadio Mane (£36m) Sunderland: Didier N’Dong (£13.6m)
Crystal Palace: Christian Benteke (£32m) Hull: Ryan Mason (£13m)
West Ham: Andre Ayew (£20.5m) West Brom: Nacer Chadli (£13m)
Leicester: Islam Slimani (£29m) Watford: Roberto Pereyra (£13m)
Southampton: Sofiane Boufal (£16m) Burnley: Jeff Hendrick (£10.5m)
Swansea: Borja Baston (£15.5m)
Klabu mbili za Manchester, City na United, zilitumia zaidi ya £150m.
Meneja mpya wa Manchester United, Jose Mourinho, alimnunua Paul Pogba kwa rekodi ya dunia £89m.
Pia walimnunua kiungo wa kati kutoka Armenia Henrikh Mkhitaryanna beki wa Ivory Coast Eric Bailly, wawili hao kwa £30m.
City, chini ya Pep Guardiola, walinunua kiungo wa kati Leroy Sane kutoka Schalke kwa £37m kisha wakalipa Everton £47.5m kumchukua beki John Stones.
Chelsea na mmiliki wao Roman Abramovich, walimpa meneja mpya Antonio Conte nguvu mpya za kutumia pesa.
Alitumia £120m, ikiwa ni pamoja na £34m kumrejesha beki Mbrazil David Luiz kutoka Paris St-Germain na £33m kumpata mshambuliaji Mbelgiji Michy Batshuayi kutoka Marseille.
Waliotawala mitandao ya kijamii
Ni mchezaji yupi aliyezungumziwa sana mitandao ya kijamii?
Ilikuwa ni difenda Mbrazil David Luiz aliyerejea Chelsea kutoka Paris St-Germain.
Kulikuwa na ujumbe 330,000 katika Twitter kumhusu, akifuatiwa na Jack Wilshere wa Arsenal, aliyetumwa kwa mkopo Bournemouth. Kulikuwa na ujumbe 108,000 kwenye Twitter kuhusu kiungo huyo wa kati.
Kipa wa Manchester City Joe Hart, aliyeenda Torino kwa mkopo, saini mpya wa Tottenham Moussa Sissoko na Samir Nasri wa Arsenal, aliyetumwa Sevilla, ndio wachezaji wengine waliozungumziwa sana.
Klabu za Ligi ya Premia zilitumia zaidi ya £155m siku ya mwisho ya kuhama kwa wachezaji kipindi cha majira ya joto na kufikisha jumla ya pesa zilizotumiwa hadi rekodi mpya ya £1.165bn.
Klabu zilikuwa tayari zimetumia jumla ya£1.005bn kufikia saa nne mchana Jumatano saa za Afrika Mashariki na kuvunja rekodi ya mwaka jana ya £870m.
Chanzo:bbcswahili.com