Jeshi la Polisi Lapeleka Kikosi Maalum Kusaka Majambazi Mkuranga

Magari ya polisi yenye zaidi ya askari 80 yakiondoka Kituo cha Polisi cha Kati, yakielekea Vikindu kwa ajili ya Operesheni saka majambazi.

Magari ya polisi yenye zaidi ya askari 80 yakiondoka Kituo cha Polisi cha Kati, yakielekea Vikindu kwa ajili ya Operesheni saka majambazi.

Askari wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wakiondoka Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati kuelekea Vikindu kwa operesheni maalumu ya kuwasaka watu wanaotuhumiwa kwa ujambazi.

Askari wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wakiondoka Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati kuelekea Vikindu kwa operesheni maalumu ya kuwasaka watu wanaotuhumiwa kwa ujambazi.

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP), Simon Sirro amesema zaidi ya askari 80 wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wameondoka leo kuelekea Vikindu na maeneo mengine ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kufanya operesheni saka majambazi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kamanda Sirro alisema askari hao zaidi ya 80 wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wanakwenda eneo la Vikindu na maeneo mengine wilayani Mkuranga mkoani Pwani kufanya operesheni ya kuwasaka watu wanaodhaniwa kujihusisha na ujambazi.

Hivi karibuni jijini Dar es Salaam inasemekana watu tisa waliokuwa kwenye pikipiki tatu walijitokeza ghafla katika Benki ya CRDB tawi la Mbande, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam na kulimiminia risasi gari la polisi lililokuwa linawasili katika eneo hilo kuleta askari kwa ajili ya lindo la usiku. Askari watatu walikufa palepale na mmoja alifia njiani wakati akipelekwa hospitali.