Kambi Tiba GSM Yaanza Kazi Iringa

Dk Shaaban, Kaimu Mkuu wa Kambi tiba ya GSM Foundation

Dk Shaaban, Kaimu Mkuu wa Kambi tiba ya GSM Foundation

Na Mwandishi Wetu
Kambi tiba inayoendeshwa na Taasisi ya Mifupa na upasuaji ya Muhimbili kwa ufadhili wa GSM Foundation inayojaribu kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi  imeanza kazi Mkoani Iringa, ukiwa ni mkoa wa nne tangu msimu wa pili wa ziara yake ya kuzunguka nchi nzima kuanza.
 
Kaimu mkuu wa kambi tioba hiyo, Daktari Bingwa Hamis Shaaban kutoka MOI amesema kwamba kwamba kumekuwa na hamasa ndogo kwa wazazi kuleta watoto wao kwa ajili ya tiba hii ya bure katika msimu huu, ukilinganisha na msimu wa kwanza ambapo jumla ya watoto 101 walifanyiwa upasuaji,
 
Katika awamu hii ya pili, mpaka leo hii ni watoto 35 wamefanyiwa, huku ukiwa ni mkoa wa mwisho kwa kambi hii kupita, hali inayoleta ukweli kwamba inaweza kumalizika bila kufikia lengo la kutibu watoto 100 na zaidi kama ilivyokuwa awamu ya kwanza.
 
Afisa habari wa GSM Foundation, Bw Khalphan Kiwamba, `Kiwadinho’, amesema sababu kuu ni wagonjwa kuwa mbali na eneo ambapo tiba inafanyika, na kambi haikuweza kusogea zaidi kwa sababu za kiufundi kwani upasuaji wa watoto hawa unahitaji maabara za kisasa ambazo zinapatikana katika Hospitali za mikoa tu.
 
Kiwamba kwa upande wake amewaomba wakazi wa iringa kujitahidi kupashana habari ili watoto wengi wapate kupata tiba hii iliyofadhiliwa tayari,
 
Kambi tiba ya GSM kwa msimu huu wa pili inamalizika Agosti 18 mwaka huu wa 2016, ambapo baada ya tathmini, tarehe za msimu wa tatu zitatangazwa.
 Mmoja kati ya watoto waliohudhuria kambi tiba ya GSM ya msimu wa pili akikaguliwa na daktari
Wataalam wakiendelea na kazi ya tiba maabara