Vijana wakiendelea kufuatilia mdahalo huo kwa makini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Msichana Initiatives Rebeca Gyumi akijibu maswali mbalimbali ambayo waliuliza vijana waliofika katika kongamano hilo na kusema kwamba sio kweli kwamba wanafunzi waliomaliza elimu ya vyuo ni vilaza.
Vijana wakiendelea kufuatilia wajibu maswali wakijibu yale waliyo yauliza.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Josephs Veronica Shayo kidato cha tano akisisitiza vijana kuwa na tabia za kuweka akiba kwa kile wanachopata ili kije kuwasaidia pindi watakapo kuwa wakubwa.
Muwezeshaji wakati wa kongamano hilo la vijana ambalo kauli mbiu yake inasema Sepesha Umasikini kwa Michongo Endelevu na yenye tija Bw. Lawrence Ambokile akiendelea kutoa mwongozo.
Noreen Toroka akijibu baadhi ya maswali lakini pamoja na hayo amewasisitiza vijana kuto kutumia kipato wanacho kipata bila tija na wawe na utaratibu wa kuhifadhi kwa ajili ya maendeleo baadae, pia aliongeza kuwa vijana wasilazie damu fursa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili yao.
Baadhi ya vijana kutoka Restless Development na wanafunzi pamoja na wadau wakendelea kufuatilia mdahalo.
Mwanzilishi wa Malkia Investment Bi. Jenipher Shigoli akichangia jambo katika mdahalo huo.
Mwanzilishi wa Charity Movement Sophia Mbeyela akitoa ushuhuda wake wa jinsi alivyo anza ujasiliamali tangia akiwa mdogo na kusisitiza kwamba vijana haijalishi ni mzima au ana ulemavu wa viungo vya mwili wake wote wanatakiwa kujumuika pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya Taifa.
Kijana Onesmo akiwaeleza vijana wenzake kuwa kama wao walemavu waviungo wanaweza kufanya mambo makubwa iweje vijana wazima wasiweze hii ilikuwa ni changamoto.