Wananchi Wafurahia Huduma za Mifuko ya Uwekezaji Nanenane Lindi.

Waziri wa Fedha Dr. Philip Mpango (Kushoto) akisalimiana na Bw. Simon Migangala Kaimu Mkurugenzi mkuu UTT AMIS wakati alipotembelea banda la wizara ya fedha katika viwanja vya NaneNane Ngongo mkoani Lindi

Waziri wa Fedha Dr. Philip Mpango (Kushoto) akisalimiana
na Bw. Simon Migangala Kaimu Mkurugenzi mkuu UTT AMIS wakati alipotembelea banda la wizara ya fedha
katika viwanja vya NaneNane Ngongo mkoani Lindi

UTT AMIS ni kampuni inayoendesha mifuko ya uwekezaji wa pamoja hapa nchini. Mpaka sasa inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha,
Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye jumla ya thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni
253.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akipata maelezo ya kina kuhusiana na mifuko ya uwekezajiwa pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS. Kushoto ni Afisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Bw. Rahim Mwanga akitoa Maelezo hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akipata
maelezo ya kina kuhusiana na mifuko ya uwekezajiwa pamoja inayoendeshwa na UTT
AMIS. Kushoto ni Afisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Bw. Rahim Mwanga akitoa
Maelezo hayo.

Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa mbadala inayowezasha watu
,vikundi, taasisi na kampuni sawa na mahitaji yao kuwekeza pesa zao kwa meneja
wa mfuko(UTT AMIS) kisha meneja huwekeza fedha hizo katika masoko ya fedha na
masoko ya mitaji kulingana na waraka wa makubaliano. Faida ipatikanayo
hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji waliofanya katika
mfuko husika.

Bi. Surah Twaakyondo, Afisa kutoka UTT-AMIS akitoa maelezo ya jinsi ya kuwekeza kwenye Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wananchi waliotembelea banda wakati wa maonyesho ya NaneNane yaliyofanyika kitaifa mkoani Lindi.

Bi. Surah Twaakyondo, Afisa kutoka UTT-AMIS akitoa
maelezo ya jinsi ya kuwekeza kwenye Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wananchi
waliotembelea banda wakati wa maonyesho ya NaneNane yaliyofanyika kitaifa
mkoani Lindi.

Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama, Ukwasi na Faida (Safety, Liquidity and Returns). Wawekezaji wote wananufaika kwakupata faida shindani hivyo kuweza kukuza mitaji yao, uwekezaji mseto hufanyika ili kupunguza hatariza uwekezaji, utalaamu wa meneja wamifuko, unafuu mkubwa wa gharama na uwazini vichocheo vinavyofanya UTT AMIS kuwa kimbilio lao. UTT AMIS – Mshirika hakika katika uwekezaji.