Sherehe za Michuano ya Olimpiki Ndani ya Jiji la Rio Brazil

oliiii

2

5.50am:Na mwenge wa Olympic uliowasili katika uwanja wa Mariccana unapokezwa aliyekuwa mwanariadha wa mbio za Marathon nchini Brazil Vanderlei Cordeiro de Lima – Ambaye anauwasha mwanga katika uwanja huo ishara ya ufunguzi rasmi ya michezo hiyo

5.32am:Wimbo wa taifa la Brazil unaimbwa kwa sasa katika ukumbi wa ufunguzi wa michezo hiyo
5.20am:Uwanja wa Mariccana ulivyofurika maelefu ya mashabiki
5.15am:Bendera zote zimewekwa pamoja kuonyesha ishara ya umoja uliopita baina ya mataifa mbali mbali duniani yanayoshiriki michezo hiyo

3

5.05am: Na sasa kikosi cha wanariadha wakimbizi pia kinaingia hapa.Baadhi ya wanariadha hawa walikuwa kule nchini Kenya wakifanya mazoezi tayari kwa maandalizi ya michezo hii.

5.00am:Kikosi cha wanariadha kinaingia kikiongozwa na bingwa katika mchezo wa tenisi Andy Murray
4.00am: Eneo la katikati la uwanja wa Mariccana limeanza kujaa wachezaji kutoka mataifa mbali mbali.

4

2.15am: Usalama uliimarishwa nje ya ukumbi wa ufunguzi wa michezo hiyo katika eneo la Barra huku vikosi vya kijeshi vikisambazwa katika kila eneo la mita 25.msongamno wa magari sio mkubwa usiku huu.Inaonekana kwamba wakaazi wa Rio wanafuatilia ufunguzi katika runinga zao majumbani mwao!

olimpik

Maandamano hayo yalioanza mwendo wa saa nane siku ya ijumaa yalikamilika katika ukumbi huo mwendo wa saa kumi na kuelekea katika uwanja wa Marrica.kulikuwa na ripoti za ghasia katika barabara inayoelekea katika uwanja huo lakini baadaye zilisitishwa na muandamanaji mmoja alijeruhiwa.

2.05am:Takriban mataifa 200 yanashiriki katika michezo hii.Sherehe hizo zimeanza kwa kurushwa kwa fataki huku mashabiki waliotoka katika seshemu mbali mbali za ulimwengu wakifurahia.

Chanzo: bbcswahili.com