NMB Yakabidhi Madawati 660 Shule Saba za Wilaya ya Kasulu

Afisa Mwendeshaji Mkuu wa NMB – Pete Novat na Afisa Tawala wa Wilaya ya Kasulu – Titus Mguha wakikagua madawati yaliyotolewa na NMB kwaajili ya shule za wilaya ya Kasulu. NMB imetoa madawati 660 kwa shule za wilayani kasulu kama mchango wa benki hiyo katika kuchangia juhudi za Rais John Magufuli ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanakaa kwenye madawati. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jana katika ukumbi wa utamaduni wilayani Kasulu.

Afisa Tawala wa Wilaya ya Kasulu – Titus Mguha akimshukuru Afisa Mwendeshaji Mkuu wa benki ya NMB – Pete Novat kwa kutoa madawati kwa shule za wilayani Kasulu. NMB imetoa madawati 660 kwa shule za wilayani kasulu kama mchango wa benki hiyo katika kuchangia juhudi za Rais John Magufuli ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanakaa kwenye madawati.Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jana katika ukumbi wa utamaduni wilayani Kasulu. Akishuhudia ni Meneja wa NMB kanda ya Magharibi – Leon Ngowi.

BENKI ya NMB imekabidhi madawati 660 kwa wilaya ya Kasulu kama mchango wake kwa serikali katika kukabiliana na uhaba wa madawati nchini. Madawati hayo yaliyogharimu kiasi cha shilingi Milioni 35 ni mahususi kwa shule za msingi tano na sekondari mbili za wilayani kasulu yenye nia ya kuwapunguzia uhaba wa madawati waliyonayo.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya madawati hayo jana, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa NMB – Pete Novat alisema kuwa Benki ya NMB ina sera mahususi ya kusaidia jamii na hutenga asilimia moja ya faida baada ya kodi kusaidia elimu nchini.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, NMB kama ilivyo katika msemo wake wa Karibu yako, imekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii hususani katika sekta ya elimu, ndio maana tumeona tusaidie shule za wilaya hii kwa kutoa madawati 660 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 35 na kuchangia kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji,” alisema Bwana Pete.

“Madawati haya tunayokabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki inayoongoza Tanzania tunahakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata.” Alisema Pete.

Bwana Pete alisema kuwa kwa Mwaka 2016, NMB imetenga Zaidi ya shilingi bilioni 1.5 kwaajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo kusaidia sekta ya Elimu, kiasi ambacho ameseka kuwa tayari kimeshatumika chote kwa kusaidia madawati nchi nzima.

Afisa Tawala wa Wilaya ya Kasulu – Titus Mguha akimshukuru Afisa Mwendeshaji Mkuu wa benki ya NMB – Pete Novat kwa kutoa madawati kwa shule za wilayani Kasulu. NMB imetoa madawati 660 kwa shule za wilayani kasulu kama mchango wa benki hiyo katika kuchangia juhudi za Rais John Magufuli ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanakaa kwenye madawati.Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jana katika ukumbi wa utamaduni wilayani Kasulu. Akishuhudia ni Meneja wa NMB kanda ya Magharibi – Leon Ngowi.

Afisa Tawala wa Wilaya ya Kasulu – Titus Mguha akimshukuru Afisa Mwendeshaji Mkuu wa benki ya NMB – Pete Novat kwa kutoa madawati kwa shule za wilayani Kasulu. NMB imetoa madawati 660 kwa shule za wilayani kasulu kama mchango wa benki hiyo katika kuchangia juhudi za Rais John Magufuli ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanakaa kwenye madawati.Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jana katika ukumbi wa utamaduni wilayani Kasulu. Akishuhudia ni Meneja wa NMB kanda ya Magharibi – Leon Ngowi.

Kwa kipindi cha Januari mpaka Juni, 2016 – NMB ilitoa madawati zaidi ya 6000 kwa shule za msingi na sekondari nchi nzima huku mwezi Julai, Ikikabidhi hundi ya shilingi Milioni 900 kwa Waziri wa Tamisemi kwaajili ya kutengeneza madawatiu zaidi ya 10,000 na kuyagawa nchi nzima.

Akipokea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Afisa Tawala wa Wilaya ya Kasulu – Titus Mguha aliwapongeza NMB na kusema kuwa kitendo chao cha kutoa misaada ya madawati kimezidi kuwapa heshima na kutoa wito kwa wakazi wa kasulu na nchi nzima kuwaunga Mkono NMB kwani ni wadau wa kweli wa maendeleo.

“Mkuu wa Mkoa amenituma niwaambie kuwa, Anawashukuru sana ten asana, NMB ni benki ambayo kila mtanzania anatakiwa kuwaunga Mkono kwani kitendo chao cha kusaidia maendeleo hususani katika elimu, ni jambo la kuingwa na kupigiwa mfano,” alisema Bwana Mguha.

Mwezi Julai, 2016, NMB ilitoa hundi kwa Waziri wa Tamisemi – Mh George Simbachawene ya shilingi Milioni 900 kwaajili ya kuunga Mkono juhudi za mheshimiwa rais wa awamu ta Tano – Mh John Pombe Magufuli ya kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi anakaa chini kwa ukosefu wa madawati nchini. Kiasi hicho cha fedha kitanunua madawati zaidi ya 10,000 yatakayogawanywa nchi nzima.