Lowasa, Waziri Nape Waongoza Wanahabari Kumuaga Joseph Senga Dar

Aliyewahi kuwa Mgombea Urais wa UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho mbele ya Mwili wa aliyekuwa mpiga picha mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima na mwanahabari mkongwe Joseph Emilio Senga, katika uwanja Sinza-Uzuri jijini Dar leo. Marehemu Senga alifariki juni 27, 2016 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Aliyewahi kuwa Mgombea Urais wa UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho mbele ya Mwili wa aliyekuwa mpiga picha mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima na mwanahabari mkongwe Joseph Emilio Senga, katika uwanja Sinza-Uzuri jijini Dar leo. Marehemu Senga alifariki juni 27, 2016 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

 


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akitoa heshima za mwisho mbele ya Mwili wa aliyekuwa mpiga picha mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima na mwanahabari mkongwe Joseph Emilio Senga,katika uwanja Sinza-Uzuri jijini Dar leo. Marehemu Senga alifariki juni 27, 2016 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akizungumza machache kabla ya kuanza kuaga Mwili wa aliyekuwa mpiga picha mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima na mwanahabari mkongwe Joseph Emilio Senga,katika uwanja Sinza-Uzuri jijini Dar leo.Mh.Nape ameeleza kuwa tasnia ya habari imempoteza mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya tasnia ya habari nchini.

 

“Joseph Senga alikuwa mwanahabari shupavu na hodari, ambaye siku zote alisimama kidete kupigania maendeleo ya tasnia ya habari na kutenda haki katika tasnia hiyo,napenda kutoa salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu” .Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) pia amewaombea wote walioguswa na kifo cha Joseph Emilio Senga kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha kuondokewa na mpendwa wao.

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura sambamba na Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,viongozi wa CHADEMA wakishiriki kutoa heshima za mwisho mbele ya Mwili wa aliyekuwa mpiga picha mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima na mwanahabari mkongwe Joseph Emilio Senga,katika uwanja Sinza-Uzuri jijini Dar leo. Marehemu Senga alifariki juni 27, 2016 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akijadiliana jambo na Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh.Saed Kubenea kabla ya kuaga mwili wa Marehemu Senga,katika viwanja vya Sinza-Uzuro jijini Dar leo,pichani Kati ni aliyewahi kuwa Mgombea Urais wa UKAWA kupitia chama cha CHADEMA (2015) na Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowassa

Mazungumzo ya hapa na pale yalikuwepo kutoka kwa viongozi wa vyama mbalimbali walioshiriki kuaga mwili wa Marehemu Senga.

Wakijadiliana jambo.

Familia ya Marehemu akishiriki kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Senga.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe mara baada ya kutoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa aliyekuwa mpiga picha mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima na mwanahabari mkongwe, Marehemu Joseph Emilio Senga, katika uwanja Sinza – Uzuri jijini Dar leo.

Mazungumzo ya hapa na pale.

 

Baadhi ya Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali wakiwa wamebeba sanduku lenye mwili wa marehemu Senga kuelekea kwenye Gari tayari kwa kuanza safari ya kuelekea mkoani Mwanza, kwa mazishi kijijini kwa Marehemu wilayani Kwimba.

 

Baadhi ya Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali wakiwa wamebeba sanduku lenye mwili wa marehemu Senga kuelekea kwenye Gari tayari kwa kuanza safari ya kuelekea mkoani Mwanza,kwa mazishi kijijini kwa Marehemu wilayani Kwimba.

 

Juu ni mke na watoto wa marehemu, Joseph Senga wakiwa katika shughuli hiyo leo.

 

Mbunge John Mnyika akitoa salamu za pole.

 

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akitoa salamu za pole.

 

Waombolezaji wakiwa pamoja na familia ya marehemu.

WAKATI HUO HUO, WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Joseph Emilio Senga na wanahabari wote nchini kufuatia kifo cha aliyekuwa mpiga picha mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima na mwanahabari mkongwe Joseph Emilio Senga kilichotokea tarehe 27 Julai, 2016 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Katika salamu zake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) amesema tasnia ya habari imempoteza mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya tasnia ya habari nchini.
“Joseph Senga alikuwa mwanahabari shupavu na hodari, ambaye siku zote alisimama kidete kupigania maendeleo ya tasnia ya habari na kutenda haki katika tasnia hiyo.
“Napenda kutoa salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu”
Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) pia amewaombea wote walioguswa na kifo cha Joseph Emilio Senga kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha kuondokewa na mpendwa wao.
RAHA YA MILELE UMPE EHE BWANA, NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE
APUMZIKE KWA AMANI
AMINA.