Mwili wa Mwanahabari Joseph Senga Wawasili Kutokea India

Baadhi ya wanahabari wakipokea jeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga, miongoni mwa waandishi waandamizi na mpiga picha mahiri nchini ulipo wasili katika uwanja wa Julias Nyerere leo jijini Dar es Salaam.

MWILI wa mpigapicha mkongwe za habari, Joseph Senga ambaye alifariki juzi nchini India alikokuwa kwa matibabu umewasilili jijini Dar es Salaam leo mchana na kupokewa na wanahabari mbalimbali katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julias Nyerere. Mwili huo mara baada ya kuwasili ulipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwa wanafamilia mwili huo leo baadae utaondolewa Muhimbili na kupelekwa nyumbani kwa marehemu Sinza-White Inn ambapo utalala hadi kesho asubuhi kwa ajili ya taratibu nyingine.

Baadhi ya wanahabari wakipokea jeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga, miongoni mwa waandishi waandamizi na mpiga picha mahiri nchini ulipo wasili katika uwanja wa Julias Nyerere leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanahabari wakipokea jeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga, miongoni mwa waandishi waandamizi na mpiga picha mahiri nchini ulipo wasili katika uwanja wa Julias Nyerere leo jijini Dar es Salaam.

Msafara wa magari yaliopokea mwili wa marehemu Joseph Senga, ulipowasili katika uwanja wa Julias Nyerere leo jijini Dar es Salaam.

Marehemu Senga aliyekuwa akifanya kazi na kampuni ya Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima kama Mkuu wa Dawati la Picha alipata umaarufu mkubwa baada ya kupiga picha tukio la kuuwawa kwa mwanahanari mahiri marehemu Daudi Mwangosi na picha zake kusaidia kiasi kikubwa kumpata muuaji wa mwanahabari hizo alipewa tuzo ya upigaji picha bora 2015.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kampuni ya Free Media mapema leo jijini Dar es Salaam, marehemu Senga ataagwa kesho Jumapili nyumbani kwake Sinza majira ya sambili asubuhi kabla ya kusafirishwa kuelekea Kwimba Mkoani Mwanza kwa mazishi yanayotarajia kufanyika siku ya Jumatatu. Mtandao huu unatoa pole kwa familia, kampuni ya Free Media na tasnia nzima ya habari nchini Tanzania. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina.