Maonesho ya Twende, Dar es Salaam Tanzania

Bango la Maonesho ya Twende

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami (katikati) akikagua baadhi ya mabanda ndani ya wajasiriamali wanawake walioshiriki katika maonesho ya Twende Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni mwaandaaji wa maonesho hayo, Mbunifu maarufu wa mavazi Tanzania, Mustafa Hassanali.

Baadhi ya washiriki wa maonesho ya wajasiriamali wanawake yanayojulikana kama TWENDE wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi katika hafla ya ufungaji maonesho hayo.