Waziri Mwigulu Nchemba Awakamata Wachina Walomtesa Kijana Mtanzania Kinyama

Waziri Mwigulu akiwa katika Gereza la Wilaya Geita akiendelea kufuatilia kwa makini tukio hilo ili kujua ukweli.

Waziri Mwigulu akiwa katika Gereza la Wilaya Geita akiendelea kufuatilia kwa makini tukio hilo ili kujua ukweli.

Wanaodaiwa kuwa ndio waliomuadhibu kijana huyo wakiwa katika gari la Polisi mara baada ya Kukamatwa.

Wanaodaiwa kuwa ndio waliomuadhibu kijana huyo wakiwa katika gari la Polisi mara baada ya Kukamatwa.

Waziri Mwigulu akiendelea kufuatilia kwa makini tukio hilo ili kujua ukweli.

Waziri Mwigulu akiendelea kufuatilia kwa makini tukio hilo ili kujua ukweli.

Picha iliyoonekana kwenye mitandao ya kijamii mtuhumiwa akiathibiwa kikatili na Wachina.

Picha iliyoonekana kwenye mitandao ya kijamii mtuhumiwa akiathibiwa kikatili na Wachina.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimuangalia kijana huyo alivyojeruhiwa.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimuangalia kijana huyo alivyojeruhiwa.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani nchini, Mwigulu Nchemba amefuatilia tukio la kijana Mtanzania anayedaiwa kuteswa na raia wa Kichina wamiliki Mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro-Geita, na kuhakikisha waliohusika na tukio hilo la kumtesa kijana wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria. Hii haoa ni kauli yake; “Nimefika Mgodi wa Nyamhuna unaodaiwa kuwa raia wa china ambao ni sehemu ya wamiliki wa mgodi huo wakishirikiana na watanzania walimtesa kinyama na kumjeruhi mmoja wa mtanzania mwenzetu aliyekuwa akifanya kazi katika mgodi huo uliopo Katoro-Geita.

“Imenilazimu kufika gereza la Geita kukutana na kijana huyo ambae yupo hai tofauti na taarifa za awali kuwa alifariki. Baada ya kujiridhisha kuanzia mavazi, majeraha, picha, sura na umbo lake kuwa ndiye kijana aliyeteswa vibaya na picha zake kusambaa mitandaoni na vyombo mbalimbali vya habari, niliamua kwenda naye hadi mgodini lilipofanyika tukio hilo la kinyama, aliwatambua wahusika ambao NI KWELI WALIFANYA TUKIO HILO LA KINYAMA NA LISILOKUBALIKI HAPA NCHINI.”

“Hivyo walioshiriki tukio hilo tumeshawashikilia kupitia jeshi la polisi tayari kwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Nalaani tukio hilo vikali sana,serikali hii ipo tayari kushirikiana na kila mmoja rai mwema kutoa taarifa popote pale za matukio au viashiria viovu na vinavyohatarisha usalama wetu. “Usalama wetu,jukumu letu sote,” anasema Waziri Mwigulu Nchemba akizungumzia tukio hilo baada ya kufika eneo la tukio.