Timu za Astra Giurgiu, Olympiacos, Viktoria Plzeň, Celtic na Dinamo Zagreb zimetinga Raundi ya 3 ya Mtoano ya UEFA , baada ya kukamilika Mechi za Marudiano za Raundi ya Pili ya Mtoano.
Droo ya Raundi ya 3 ya UCL ilifanyika na kuhusisha Miamba ya Ajax, Steaua, Olympiacos, Shakhtar, Anderlecht na Fenerbahçe. Monaco iliyomaliza Nafasi ya 3 kwenye Ligi 1 huko ufaransa , na Timu za Pili za Ligi za Nchi za Ulaya ambazo ziko Nafasi za 7 hadi 15
kwenye Listi ya Ubora ya Nchi Wanachama wa UEFA.
Droo ya Pili ni kwa timu za Mabingwa iliyohusisha Washindi 17 kutoka Raundi ya Pili ya Mtoano ya UCL pamoja na Mabingwa wa ugiriki, Jamhuri ya Czech na Romania.
Washindi wa Raundi ya 3 ya Mtoano wanasonga mbele na kuingia Raundi ya Mwisho ya Mchujo ambayo ni Hatua moja kabla ya Makundi.Timu zitazoshindwa Raundi ya 3 ya Motoano zitatupwa kwenye Hatua ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo wa UEFA ligi barani ulaya.
na Usiku wa Julai 21 Genk ilikuwa uwanja wa ugenini kuikabili timu ya Buducnost kwenye michuano ya kuwania kupangwa hatua ya makundi ya michuano ya Europa League.
Katika mchezo huo uliomalizika kwa kwa Genk kufungwa bao 2-0, ilibidi umauliwe kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 30 za nyongeza kumalizika kwa matokeo ya 2-0 yaliyosabaisha matokeo ya jumla kuwa sare ya 2-2.
Ikumbukwe mchezo wa awali (Julai 14) takriban juma moja lililopita Genk ilipata ushindi wa magoli 2-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani huku Samatta akifunga bao la pili.
Samatta akicheza kwa dakika zote 120, alifunga moja ya penati ambazo ziliisaidia timu yake kusonga mbele kwenye michuano hiyo. Mikwaju ya penati kwa upande wa Genk ilifungwa na Dries Wouters, Mbwana Samatta, Bryan Heynen na Thomas Buffel na kuvusha Genk kwenda raundi ya pili kwa jumla ya penati 4-2.
Genk itapambana na klabu ya Cork City kutoka Jamhuri ya Ireland katika raundi ya pili ya kutafuta tiketi ya kucheza Europa League hatua ya makundi.
chanzo: shaffihdauda.co.tz