Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kabla ya kuondoka katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akiagana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya kuondoka jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akipungia mkono vikundi vya utamaduni vilivyokuwa vikitoa buradani katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Rais Magufuli wakiwa na watoto wa Kitanzania wenye asili ya kihindi kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akishukuru kabla ya kuondoka baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
Picha na Ikulu