Soko Lachafuka Arsenal, Man City, Chelsea Wavuta Vifaaa Vipya

A

Arsenal wamekubali kumsajili mshambulizi chipukizi kutoka Japan Takuma Asano. Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 21 amejiunga na the Gunners akitokea klabu ya nyumbani ya Sanfrecce Hiroshima.

Kandarasi yake hata hivyo itakamilishwa baada ya kufanyiwa vipimo vya afya. Arsenal imechapisha kwenye tovuti yake picha za mashambulizi huyo na kumkaribisha uwanjani emirati. Takuma amewahi kuichezea Japan katika mechi 5 za kimataifa.

Takuma anatarajiwa kujumuishwa katika kikosi cha nchi hiyo kitakayoshiriki michezo ya Olimpiki mwezi ujao jijini Rio de Janeiro Brazil.

Takuma amecheza mechi 56 na kufunga mabao 11 katika ligi kuu ya Japan J-League. Alishinda ligi hiyo ya J1 League mwaka wa 2013 na 2015, Japanese Super Cup 2013, 2014 na 2015,mwaka huo pia alituzwa kama chipukizi bora wa mwaka .

Kocha Arsène Wenger amemsifu mshambulizi huyo kwa ukakamavu wake

b

Nao Chelsea wameshamsajili mshambuliaji Michy Batshuayi kutoka Marseillekwa mkataba wa miaka mitano.

Kijana huyo mbelgiji wa miaka 22 anakuwa wa kwanza kununuliwa na meneja mpya pale Stamford Bridge.

Antonio Konte. Malipo hayajawekwa wazi lakini inaaminika kuwa ni pauni milioni 33 sawa na Euro milioni 40. Manchester United wamewaambia Juventus kuwa wako tayari kulipa pauni milioni 100 kumsajili kiungo kutoka Ufaransa Paul Pogba, 23, na watampa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki (Mail on Sunday).

Arsenal watampa mkataba mpya Arsene Wenger kwa matumaini ya kumshawishi asiondoke baada ya tetesi kuzagaa kuwa chama cha soka cha England, FA, kinamnyatia (Observer).

Meneja mpya wa Manchester City, Pep Guardiola anataka kumsajili mshambuliaji kutoka Uruguay anayeichezea Barcelona, Luis Suarez, 29, anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 85, pamoja na kiungo Mjerumani anayechezea Real Madrid, Toni Kroos, 26, ambaye kipengele chake cha uhamisho kina thamani ya pauni milioni 63 (Sunday Mirror).

Mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain wamekubali kumsajili kiungo kutoka Poland anayechezea Sevilla Gregorz Krychowiak, 26, kwa pauni milioni 22 (Marca).

Liverpool watapambana na Everton katika kumsajili kiungo kutoka Ubelgiji Axel Witsel, 27, anayecheza soka Zenith St Petersburg nchini Urusi (Sunday Mirror).

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Arsenal, Robin van Persie, 32, huenda akarejea katika ligi kuu ya England baada ya klabu yake ya sasa Fernabahce ya Uturuki kuwaambia West Ham na Crystal Palace kuwa wanaweza kumsajili (Sun on Sunday).

Chelsea wamefanikiwa juhudi za kumsajili beki kutoka Senegal, Kalidou Koulibaly, 25, anayechezea Napoli kwa pauni milioni 30 (Sunday Mirror).

Tottenham wanajiandaa kutoa pauni milioni 38, kumtaka mshambuliaji wa Inter Milan, Mauro Icardi, 23, na tayari wamepeleka wawakilishi wao Italy kuzungumza na mchezaji huyo kutoka Argentina (GianlucaDiMarzio), kipa wa Spurs Hugo Lloris, 29, ananyatiwa na Real Madrid kwa pauni milioni 35 (Sunday Mirror).

Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino yuko tayari kumuuza Ryan Mason, 25, kwenda Hull City iliyopanda daraja kwa pauni milioni 10 (Sun on Sunday), kiungo wa Watford Jose Manuel Jurado, 30, amehusishwa na kuhamia Espanyol na kuungana na meneja wake wa zamani Quique Sanchez Flores (Fichajes).

Middlesbrough watakamilisha usajili wa pauni milioni 11.75 wa kiungo kutoka Atalanta, Marten de Roon, 25, baada ya kukubaliana maslahi binafsi na mkataba wa miaka minne (Gazette),

Timu nne za EPL zimekuwa zikiwasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Wales, Hal Robson Kanu tangu alipopachika bao dhidi ya Ubelgiji kwenye michuano ya Euro 2016.

Kanu ni mchezaji huru baada ya kuachiliwa na klabu yake ya Reading (Sky Sports).

Stoke huenda wakalazimika kulipa takriban pauni milioni 20 kama wanataka kumsajili mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22 (Stoke Sentinel).