Mwanahabari Omary Masoud wa Azam Media Azikwa Jijini Dar

Mwili wa marehemu Omary Masoud aliyekuwa mfanyakazi wa Azam Media ukipelekwa makaburini tayari kwa mazishi.

Mwili wa marehemu Omary Masoud aliyekuwa mfanyakazi wa Azam Media ukipelekwa makaburini tayari kwa mazishi.

 

 Baadhi ya wafanyakazi wa Azam Media wakiwasili katika Msikiti wa Maamur uliopo Upanga Jijini Dar es Salaam ambapo mwili wa marehemu Omary Masoud uliswaliwa. Marehemu Omary alifariki dunia Julai 2 kwa ajali ya gari katika eneo la Boko. 
 Waombolezaji wakiwa Msikitini Upanga.
Mwili wa marehemu ukitolewa Msikitini kwa ajili ya maziko.
Baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakishirikiana na ndugu wa marehemu kubeba mwili wa marehemu.
Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa nyumbani kwao Boko. 
Mwili wa marehemu ukiombewa dua. 
 
Waombolezaji wakiomba dua kwa ajili ya marehemu.
Ndugu na jamaa wakiwa nyumbani kwa marehemu. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari pamoja na ndugu wa marehemu. 
 Ndugu wa marehemu wakiusubiri mwili kuwasili makaburini.
 Kaka wa marehemu Salehe Masoud (wapili kulia) akiwa na baadhi ya ndugu walioshiriki maziko.
Mwili wa marehemu ukishushwa kaburini. 
Mwili wa marehemu ukiingizwa kaburini. 
Kaka wa marehemu Salehe Masoud (katikati) akishiriki maziko ya mdogo wake. 
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa na huzuni wakati mwili ukishushwa kaburini.
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga akiweka udongo katika kaburi la marehemu Omary.
Ndugu wa marehemu wakiweka udongo kwenye kaburi. 
Mkurugenzi wa Azam Media, Abubakar Bakhresa (wakwanza kulia) akifuatiwa na Azizi Salumu, Kamanda Mpinga na Awadhi Salum.
 Ndugu wakimuimbea dua marehemu baada ya maziko.
Kamanda Mpinga akimpa pole kaka wa marehemu, Salehe Masoud. 
Kaka wa marehemu Salehe Masoud (katikati) akipewa pole na Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama. (Picha na Francis Dande)