Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeondoka leo jijini Dar es Salaam alfajiri ya saa 9 kuelekea Seychelles kwa ajili ya mchezo wao wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Julai 2.
Kikosi cha Serengeti Boys kinatarajiwa kuwasili Seychelles majira ya saa 9 alasiri huku mchezo wao ukitarajiwa kuchezwa saa 10:00 kwa saa huko.
Kikosi kinaundwa na wachezaji 20, benchi la ufundi lina watu sita, wajumbe wawili wa kamati ya utendaji, afisa habari pamoja na mshauri wa maendeleo ya soka la vijana Bw. Kim Polsen, daktari wa timu na kit manager.
Kwenye mchezo wa awali uliochezwa kwenye uwanja wa taifa, Serengeti Boys walipata ushindi wa magoli 3-0 hivyo wanahitaji ushindi au sare yeyote ili kufuzu kwa raundi inayofuata.