Kocha Kally Ongala ataendelea kubaki kuwa kocha mkuu wa Majimaji baada ya klabu hiyo baada ya kumpa mkataba mpya huku wakijiandaa kwa ajili ya msimu ujao
Klabu ya Majimaji FC, imekamilisha dili lake la kumpa mkataba mpya kocha wake Kally Ongala na sasa ataendelea kuifundisha timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu ujao.
Mwenyekiti wa timu ya Majimaji Hamfrey Milanzi, alisema, wamemalizana na kocha huyo na sasa wanapambana katika usajili ili kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.
Ongala alikabidhiwa kikosi cha Majimaji kikiwa kinaburuza mkia na pointi 11 baada ya kucheza mechi 13, lakini akapigana na kufanikiwa kumaliza ligi nafasi ya kumi baada ya kujikusanyia pointi 35.