WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame M. Mbarawa, leo tarehe 25 Juni, 2016 amemteua Mhandisi Deusdedit Conatus Vitalis Kakoko kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa wanahabari na Wizara wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, na kusainiwa na Kaimu Katibu wa Waziri wa wizara hiyo, Ramsey Kanyanga imesema Mhandisi Kakoko amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Ephraim Mgawe ambae uteuzi wake ulitenguliwa. Mhandisi Kakoko ni Meneja wa miradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Uteuzi huu unaanza mara moja.