Wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, Yanga ya Jangwani usiku wa kuamkia leo walikumbana na kibano cha bao moja kwa bila kutoka kwa Bejaiya ya Algeria.
Yassin Sahli ndiye aliyewapa machungu wanajangwani dakika ya 20 tu pale alipoifungia timu yake bao bekee kwenye mchezo huo lililodumu kwa dakika zote za mchezo huo
Mabingwa wa msimu ulipita Ligi ya Mabingwa Afrika, TP Mazembe nayo imeanza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho kwa kishindo baada ya kutoa kipigo cha mabao 3-1 kwa wageni wake, Medeama kutoka Ghana.
Yanga watalazimika kuzikata kilomita 6120 kurejea kwao Tanzania kabla ya kujipanga kukutana na Kisiki kingine TP Mazembe ya DRC.