Wanafunzi Chuo Kikuu SMMUCo Watembelea Hifadhi ya Ngorongoro

Simba jike akiwa amelala kwenye nyasi zinazoendana na rangi yake katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

Simba jike akiwa amelala kwenye nyasi zinazoendana na rangi yake katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

 

Simba dume  akiwa anaunguruma
 

 

Na Dickson Mulashani, Ngorongoro
 
SUALA la utalii wa ndani limeonekana kupata mashiko baada ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Stefano Moshi Memorial University College (SMMUCo) kuhamsika na kuamua kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ili kujionea vivutio vya kipekee vinavyopatikana humo.
Akizungumzia safari hiyo mmoja wa wanafunzi hao Emmanuel Kalenzi amesema waliguswa kupanga ziara hiyo kuunga mkono wadau mbali mbali wanaohamasisha utalii wa ndani ili kuweza kuwa mabalozi kwa wengine. “Sisi kama wasomi ndio tunapaswa kuwa mabalozi kwa jamii inayotuzunguka na ili uwe balozi mzuri basi uwe umashajionea kwa macho,”  alisema.

Nyati dume mwenye umri mkubwa ambaye tayari ametengwa na kundi lake.
Ndege aina ya Cranes nao wanapatikana katika eneo la crater

 

Nyumbu akiwa amepumzika mara…
 Wanafunzi hao wakiwa katika geti la kuingia hifadhi ya Ngoro ngoro

Wanafunzi hao wakiwa katika geti la kuingia Hifadhi ya Taifa Ngorongoro