Bondia Muhammadi Azikwa Kama Mfalme

ali

Maelfu ya watu wamemuaga aliyekuwa bondia shupavu Muhammad Ali nyumbani kwake katika mji wa Louisville huko Kentucky.

Bondia wa Uingereza Amir Khan ambaye alikutana na Muhammed Ali mara mbili alisema kuwa Ali alikuwa kielelezo chake.Ali alikuwa na pande nyingi lakini unapoangalia mafanikio yake katika ndondi kwa kweli ni makubwa mno,alisema.

Watu walijipanga kandokando ya barabara huku msafara wa gari lililobeba mwili wa Ali ukiendelea kupita katika maeneo muhimu ya Ali wakati wa maisha yake huku baadhi ya mashabiki wake wakimsifu Ali! Ali !

Kushindwa kwa rais wa Uturuki Tayyip Erdogan kuhudhuria mazishi ya Muhammad Ali licha ya kufunga safari nchini Marekani kuhudhuria kumeangaziwa na magazeti mengi ya Uturuki imeleta picha ya tofauti

Kuwepo kwa maelfu ya watu katika mazishi ya Muhhamad Ali wakiwemo viongozi kutoka mataifa tofaut duniani kunaonyesha umuhimu wake duniani kama shujaa.