SHIRIKA la ‘Red Crescent organisation’ limesema kuwa idadi ya miili ambayo imepatikana hadi sasa katika ufukwe wa bahari Magharibi mwa Libya imeongezeka na kufikia miili 117. Taarifa zinadai waliofariki wanaaminika walikuwa ni wahamiaji kutoka Jangwa la Sahara ambao walikufa maji wakijaribu kuelekea Ulaya.
Hata hivyo haijulikani ni lini wahamiaji hao haramu walikufa maji katika safari yao. Miili ya wahamiaji hao ilibebwa na maji na kuachwa katika ufukwe wa mji wa Zuwara, ambapo maboti mengi yalio hafifu baharini yanadaiwa kuondoka kueleka Italy yakiwa yamejaa wahamiaji.
-BBC