Klabu ya Manchester City imemsajili kiungo wa kati wa Ujerumani IIkay Gundogan kutoka kwa kilabu ya Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka minne.
Mchezaji huyo wa miaka 25 ambaye hatoshiriki katika michuano ya Euro 2016 pamoja na kuanza kwa ligi ya Uingereza msimu huu kutokana na jeraha atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa kilabu ya Mancity Pep Guardiola.
Manchester City imeripoti kulipa kitita cha pauni milioni 20 kumpata Gundogan. Nilipogundua kwamba City walikuwa wakinihitaji,moyo wangu ulikubali”,alsiema.”Mambo yamenda haraka sana”.
Mkurugnzi wa klabu hiyo ya Ligi ya Uingereza Txiki Begiristain alipongeza maadili ya Gundogan pamoja na uwezo wake
Naye Beki wa kulia wa Brazil Dani Alves anaondoka Barcelona, kulingana na klabu hiyo. Alves mwenye umri wa miaka 33 alijiunga na Seveilla mwaka 2008 na kushinda mataji 3 ya ligi ya vilabu bingwa pamoja na mataji sita ya La Liga na Barcelona.