Yadi ya Mabasi ya UDA Yanusurika Kuteketea kwa Moto

Eneo la nje ya yadi ya mabasi ya UDA iliyopo Mbagala Rangi Tatu lililokumbwa na moto baada ya kuangukiwa na moja ya nguzo ya umeme inayosafirisha umeme mkubwa jirani na eneo hilo.

Eneo la nje ya yadi ya mabasi ya UDA iliyopo Mbagala Rangi Tatu lililokumbwa na moto baada ya kuangukiwa na moja ya nguzo ya umeme inayosafirisha umeme mkubwa jirani na eneo hilo.

Moja ya nguzo za TANESCO zilizoanguka na kuzua moto kwenye yadi ya UDA, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Moja ya nguzo za TANESCO zilizoanguka na kuzua moto kwenye yadi ya UDA, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wananchi wakiwa wamekusanyika moja ya eneo nje ya yadi ya UDA kuangalia tukio la kuzuka moto katika moja ya majengo ya yadi hiyo.

Baadhi ya wananchi wakiwa wamekusanyika moja ya eneo nje ya yadi ya UDA kuangalia tukio la kuzuka moto katika moja ya majengo ya yadi hiyo.

YADI ya mabasi ya UDA iliyopo eneo la Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam imenusurika kuteketea kwa moto baada nguzo inayosafirisha umeme mkubwa barabarani kuangukia uzio wa yadi hiyo na kusababisha shoti kabla ya kuanza kuwaka moto baadhi ya majengo ya yadi hiyo. Moto huo ulioanzia kwenye nyaya za umeme baada ya kuanguka kwa nguzo na kukatika kwa nyaya ulianza kuenea kwenye moja ya jengo la yadi hiyo huku wafanyakazi na walinzi wa yadi hiyo wakijitahidi kuuzima, kabla ya kuomba msaada TANESCO.

Jengo lililoshika moto lilionekana likitoa moshi mkubwa juu huku baadhi ya kuta zikiwaka moto kwenye paa za jengo hilo. Kikosi cha dharura cha TANESCO kiliwahi kufika eneo hilo na kukata umeme katika moja ya mitambo inayoleta umeme eneo hilo hivyo kupunguza kasi ya kueneo kwa moto huo. dev.kisakuzi.com ilishuhudia baadhi ya wafanyakazi wakiangaika kuuzima moto huo huku gari la doria la Jeshi la Polisi likiangalia usalama eneo hilo pamoja na kusaidia kuzuia moto kuenea.

Hata hivyo walifanikiwa kuuzima moto huo. Haikujulikana mara moja athari ya moto huo ndani ya yadi hiyo baada ya baadhi ya wafanyakazi waliohojiwa kugoma kuzungumzia tukio hilo kwa madai si wasemaji wa yadi hiyo.