Rais Magufuli Ateuwa Naibu Mwanasheria, Mshauri Wake Kiuchumi

Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Rais Dk. John Pombe Magufuli.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk).

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari; Bw. Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Tulia Ackson ambaye amechaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi.

Kabla ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo tarehe 23 Mei, 2016 imeeleza kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.