Pombe Yamfukuzisha Kazi Waziri wa Magufuli

Waziri Charles Kitwanga.

Waziri Charles Kitwanga.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kwa kuingia bungeni akiwa mlevi. Kwa mujibu wa taarifa ya Rais Magufuli kwa vyombo vya habari kutoka Ikulu, amefikia hatua hiyo baada ya kubainika Charles Kitwanga aliingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa mlevi.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016. Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kufuatia kitendo cha Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa,” imesema taarifa ya Rais kutoka kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu.