Na Dotto Mwaibale
CHAMA Cha Wakadiriaji Majengo Tanzania (TIQS) kwa kushirikiana na Chama cha wakadiriaji majenzi Afrika (AAQS), watakuwa wenyeji wa mkutano mkuu wa Wakadiriaji Majenzi wa Afrika utakaofanyika tarehe 18 na 19 Agosti 2016 jijini Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine chama hicho kimemuomba Rais John Magufuli,awape kazi katika miradi ya ujenzi, ili aweze kupunguza upotevu wa fedha unaotokana udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Rais wa TIQS, Samweli Marwa alisema kuwa, wamesikia kilio cha Rais kuhusu ufisadi unaotokea katika miradi mbalimbali ya ujenzi hapanchini, na kusababishia hasara kubwa Serikali.
‘’Sisi tuko tayari kutumia taaluma yetu,
ilikumsaidia RaisMagufuli, kwani watu wamezidi kudanganya kwa lengo la
kujinufaisha wenyewe’’ alisema.
Marwa alisema, Rais akiwatumia wao wataweza kupunguza gharama za ujenzi,
pamoja na kujua gharama kabla ya kuingia mikataba mbalimbali. Alisemakuwa, huduma ya ukadiriaji majengo ni nguzo muhimu katika kuchangia ufanisi na udhibiti wa gharama za ujenzi, ikiwa pamoja na ukamilishaji kwa muda wa miradi na kupata thamani ya fedha.
Marwa alisemawao kazi yao, wanatathmini kabla ya kujenga hivyo Rais atakuwa na uhuru wa kukubali mradi au lah, endapoataonagharamaimekuwakubwa.
Wakati huo huo Chama hicho, kimemuomba Magufuli kuwa mgeni rasmi katika mkutano Mkuu wa Afrika wa wakadiriaji majengo unaotarajia kufanyika Agosti 18 na 19 Jijini Dar es Salaam.
Marwa alisema kuwa, kwa kutambua umuhimu wakazi yao katika Taifa hili,
wameona ni vema kama Rais angekuwepo katika mkutano huo iliaweze kujua mambo
mbalimbali yahusuyo chama hicho.
Alisemakuwa, mada Kuu katika mkutano huo ni’ kufikiaMalengo endelevu(SDGs)-
mchango wahuduma za ukadiriaji majengo’ yanayokusudia kuondoa umaskini, kupambana na udhalimu, kuleta usawa pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.