Mchezaji wa Soka Afariki Dunia Akiwa Uwanjani

download

Mchezaji wa soka la kimataifa eraia wa Cameroon, Patrick Ekeng, amefariki baada ya kuanguka uwanjani katika ligi ya Romania.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alipoteza fahamu dakika saba tu baada ya kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine katika timu yake ya Dinamo Bucharest katika mji mkuu wa taifa hilo, Bucharest.

Hakuwa amegusana wala kukaribiana na mchezaji mwingine alipoanguka uwanjani.

Matabibu walimkimbiza hospitalini ambako madaktari walijaribu kumfufua kwa zaidi ya saa moja bila kufaulu.

Kwa muda wa miaka michache iliyopita wachazaji kadhaa Waafrika wamefariki walipokuwa wakicheza uwanjani.