Tanzania imekuwa ya mwisho Afrika Mashariki katika orodha iliyotolewa na shirikisho la soka duniani Fifa baada ya kushika nafasi 129 duniani huku ikishika mkia miongoni mwa mataifa ya Afrika Kusini.
Taifa linaloongoza katika eneo hili la Afrika ni Uganda ikiwa katika nafasi ya 72,Rwanda katika nafasi ya 87,Kenya katika nafasi ya 116 na Burundi katika nafasi ya 122.
Nayo Argentina bado inaendelea kuongoza katika orodha hiyo ikifuatiwa na Ubelgiji na baadaye Chile katika nafasi ya tatu.
Mabingwa wa kombe la dunia Ujerumani wanashikilia nafasi ya 5 huku Uhispania na Brazil zikifuata katika nafasi ya tano na sita mtawalia.Timu ya taifa ya Argentina bado inaongoza orodha ya kila mwezi ya FIFA ya timu bora duniani ambayo imetolewa jana Ijumaa.
Kwenye orodha hiyo timu ya taifa ya Ubelgiji iko kwenye nafasi ya pili ikifwatiwa na Chile.Ujerumani ni ya 5,ikifwatiwa na Uhispania na Brazil inachukua nafasi ya saba.
Timu ya bara la Afrika inayochukua nafasi nzuri kwenye orodha hiyo ya FIFA ni Algeria iliopo katika nafasi ya 33 ikifwatiwa na Ivory Coast katika nafasi ya 34.
Kwa nchi za Afrika mashariki Uganda 72;Rwanda 87 kenya 116 Burundi 122 na Tanzania inachukua nafasi ya 129 kwenye orodha hiyo ya FIFA