Na Mwandishi Maalumu
RAIS wa Comoro Dk. Ikililou Dhoinine anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania leo Septemba 15, 2011 kufanya ziara ya kikazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu Dk. Dhoinine atawasili majira ya mchana na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Ratiba na taarifa zaidi ya ziara yake itatolewa na mtandao huu mara itakapotufikia.