Mitandao ya Kijamii Yatishia Amani Magazeti ‘Print Media’

Mitandao ya Kijamii Yatishia Amani Magazeti 'Print Media'

TAARIFA ya utafiti inaeleza kuwa vyombo vya habari vya asilia hususan magazeti vinakufa kadri teknolojia ya upatikanaji habari inavyo kuwa. Hivi sasa vyombo vingi vya aina hiyo vinajikongoja kutokana na  mauzo hafifu na mdororo wa mapato upandea wa matangazo jambo linalovilazimu kupunguza wafanyakazi. 

Kwa mujibu wa utafiti wa ‘Pew Research Centre’ unabainisha kuwa wakati idadi ya wasomaji wa habari za magazeti ya kawaida ‘wamakaratasini’ ikishuka, idadi ya wasomaji wa habari za mtandaoni inazidi kukua huku wanaoperuzi mtandaoni  kuonekana hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando. 

Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 (“State of the News Media 2015,”) imeonesha kwamba vyombo vya habari vya magazeti (print media) ‘makaratasini’, Digitali na TV, vimeonesha dhahiri kwamba magazeti yanaelekea kutoweka. 
Utafiti huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa mtandaoni wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa ‘print media’, ambapo gazeti kubwa la New York Times la Marekani limetangaza kuwa nakala zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali na idadi ya wasomaji wa mitandaoni. 
 Hivi sasa kuna mjadala mitandaoni endapo kama Tanzania iko ama itafika huko. Mabishano ni makali ambapo wa makaratasini wanashikilia msimamo wao kuwa nchini hapa tasni ya habari mtandaoni bado ni changa sana kuweza kutishia amani ya magazeti. 
Lakini kwa upande wa digitali unajibu kwamba endapo kama kuna wahariri viburi wanaobeza kasi ya mitandao, basi wakae mkao wa kulala njaa muda si mrefu ujao, maana ni wachache wanaoendelea kupata habari kwa njia asili ya magazeti. 
Upande wa digitali umeyasifia magazeti ya Global Publishers na la Mwananchi  anbayo ni dhahiri yana wahariri wanaokwenda na wakati na wanaojua nini wanachokifanya kwa kuanza na mapema kuogelea bahari ya maendeleo ya tasnia kwa vitendo kwa kuwa na vitengo vya mtandao vinavyopelekesha mbio magazeti yanayobeza technolojia hio kwa kubuni.
“Ni kweli kwamba Tanzania ni bado sana kiteknolojia na miundombini kiasi cha habari za mtandaoni zikatishia uhai wa habari za makaratasini, lakini si uwongo kwamba ukizingatia uharaka na gharama pamoja na kwenda na wakati muda si mrefu print media itakwenda na maji”, amesema blogger mmoja ambaye pia ni mwanahabari kwenye moja ya magazeti makubwa nchini.