Kamati ya Nidhamu ya TFF Kukaa Kesho

mvella

Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kinafanyika kesho Jumanne Mei 3, 2016 kwenye ukumbi wa ofisi za shirikisho zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho cha kupitia mashauri mbalimbali yaliyowasilishwa TFF, ilikuwa kifanyike Jumapili Mei Mosi, lakini kiliahirishwa kwa sababu ya wajumbe wengi walikuwa na udhuru.

Wadau watakaojadiliwa kesho ni pamoja na Kocha Mkuu wa Azam FC ya Dar es Salaam, Stewart Hall na wachezaji wake wakiwamo John Bocco, Shomari Kapombe, Aishi Manula na Kipre Tchetche.

Wengine ni nyota wa Young Africans SC ya Dar es Salaam ambao ni Amissi Tambwe na Donald Ngoma wakati kutoka timu ya JKT Rwakoma ya Mara wamo Paulo Jinga, Zephlyn Laurian na Idrisa Mohamed.

Wengine ni Ismail Nkulo, Said Juma, Idd Selaman na Edward Amos wa Polisi Dodoma, kadhalika Abel Katunda wa Transit Camp ya Dar es Salaam na daktari wa Coastal Union ya Tanga, Dk. Mganaga Kitambi.

Pia Herry ‘Mzozo’ Chibakasa wa Friends Rangers ya Dar es Salaam naye atajadiliwa na Bunu Abdallah ambaye ni Kocha Msaidizi wa JKT Oljoro ya Arusha.